TAASISI YA KUELIMISHA WANAWAKE YA USAMBARA MAGHARIBI

 

 

 

 

  TAASISI YA UELIMISHAJI WANAWAKE YA USAMBARA MAGHARIBI******KUMUELIMISHA MWANAMKE NI KUIELIMISHA JAMII NZIMA!

Wednesday, March 21, 2007

MAELEZO KUHUSU WUWE

West Usambara Women Education (WUWE)
Taasisi ya Kuelimisha Wanawake ya Usambara Magharibi.


Taasisi hii ilianzishwa mnamo mwaka 1999, kama taasisi ya kijamii isiyo ya kiserikali (CBO). Ilianzishwa na wanachama kumi na sita walio katika Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Pamoja na kwamba mwanzoni taasisi hii ilikuwa inafanya kazi zake katika Usambara magharibi tu (Lushoto na Korogwe), kwa sasa shughuli za taasisi hii zimesambaa katika mikoa mbali mbali, kutokana na mahitaji ya huduma zake kwa jamii kuongezeka. Mpaka sasa tumefanya kazi katika mikoa kadhaa ya Tanzania bara kama vile Kagera, Mbeya, Morogoro, Pwani, Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Taasisi hii imesajiliwa na Wizara ya Mambo na Ndani ya Nchi ikiwa na namba ya Usajili SO. No. 11624.

Utume Wa WUWE
Kwanza, ni kutoa elimu ya utawala na ujasiriamali kwa wanawake, katika shughuli zao za kujiongezea kipato. Pili, kutoa elimu ya utunzaji na ustawishaji wa mazingira katika jamii, kama vile matumizi bora ya ardhi, matumizi bora ya maji katika maeneo mablimbali, hasa yale yaliyo na kilimo cha umwagiliaji, utunzaji wa misitu na vyanzo vya maji. Matumizi bora ya bidhaa za misitu na majiko sanifu. Tatu, kushirikiana na taasisi nyingine katika kuielimisha jamii juu ya kujikinga na magonjwa mbali mbali kama vile tauni, ukimwi, kipindupindu na ugonjwa wa matumbo. Nne, kuwawezesha wanawake kupata mikopo katika taasisi za kifedha kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao. Tano, kufanya tafiti mbali mbali na kutoa machapisho ambayo yatasaidia kuboresha hali ya maisha ya wanawake.

Uzoefu
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999, WUWE tumefanya kazi mbali mbali katika jamii, hasa ujenzi wa majiko sanifu ya “Ukombozi” yanayotumia kuni kidogo sana. Pia tumetoa elimu ya upandaji na utunzaji miti kwa vijiji mbali mbali vya wilaya ya Lushoto. Tumekuwa tukihudhuria warsha na makongamano mbali mbali ya ndani na nje ya nchi zinazohusiana na kazi zetu, kama vile utunzaji wa mazingira na ujenzi wa majiko bora, nchini Ujerumani, Kenya na Malawi. Pia tunaendesha semina na makongamano mbali mbali kuhusu ujasiriamali, utunzaji wa mazingira na ujenzi wa majiko sanifu.

Mafanikio
Taasisi ya WUWE imefanikiwa kutimiza malengo yake mbali mbali. Kuhusu majiko sanifu ya ukombozi, tumejenga majiko 7516. Idadi hii ni katika wilaya ya Lushoto tu, hivyo haihusishi majiko yaliyojengwa katika mikoa mingine iliyotajwa hapo juu. Katika maeneo ambayo tumejenga haya majiko sanifu, kiwango cha uharibifu wa mazingira kimepungua sana, ukilinganisha na miaka na nyuma. Hali hii inatokana na majiko haya sanifu kutumia kuni kidogo sana, hivyo kupunguza safari za mara kwa mara kutafuta kuni na kuokoa muda na mazingira. Tumetoa mafunzo ya ujenzi wa majiko sanifu kwa wanawake 498 katika vijiji 45 katika ya vijiji 162 vya wilaya ya Lushoto. Hawa wamepata vyeti vya kufuzu mafunzo na wanafanya kazi pia kama wakufunzi katika kufundisha mafundi wapya. Nje ya wilaya hii, tumetoa mafunzo kwa wanawake 104 juu ya ujenzi wa majiko sanifu.
Mnamo Desemba mwaka 2003, jiko la Ukombozi lilishinda tuzo ya kimataifa ya UNIFEM (United Nations Development Fund for Women).

JINA LETU: WUWE
MAHALI TULIPO: LUSHOTO, TANGA, Tanzania
KUHUSU WUWE:
ZAIDI

YALIYOMO

MASKANI
WANACHAMA WETU
WASILIANA NASI

WASHIRIKA WETU

WANACHAMA WETU
TaTEDO
HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO
CAMARTEC

WORLD DAY OF PRAYER
GDS

WUWE

Karibu katika tovuti hii ya WUWE. Hapa tutakuwa tunaweka mada mbali mbali ambazo zinahusiana na kazi zetu, ambazo lengo lake ni kuwasaidia wanawake kwa namna mbalimbali, hasa katika masuala ya elimu na ujasiriamali. Tunaamini kuwa kumwelimisha mwanamke ni kuielimisha jamii nzima, hivyo tukisaidiana kutoa elimu tunaamini tutafanikiwa.

HIFADHI

WUWE





 

MSANIFU: MWALYOYO


©WEST USAMBARA WOMEN EDUCATION (WUWE) 2007. All rights reserved.